Skip to content
Merged
Show file tree
Hide file tree
Changes from all commits
Commits
File filter

Filter by extension

Filter by extension

Conversations
Failed to load comments.
Loading
Jump to
Jump to file
Failed to load files.
Loading
Diff view
Diff view
Original file line number Diff line number Diff line change
@@ -0,0 +1,94 @@
---
title: Jinsi ya kutambua tokeni za udanganyifu
description: Kuelewa tokeni za udanganyifu, mbinu zinazo zifanya zionekane kuwa halali, na jinsi ya kujiepusha nazo.
lang: sw
---

# Jinsi ya kutambua tokeni za ulaghai {#identify-scam-tokens}

Moja ya matumizi yanayojulikana sana ya Ethereum ni pale kikundi cha watu kinapotengeneza tokeni inayoweza kuuzwa, kwa maana nyingine, sarafu yao wenyewe. Tokeni hizi kwa kawaida hufuata kiwango, [ERC-20](/developers/docs/standards/tokens/erc-20/). Hata hivyo, popote palipo na matumizi halali yanayoleta thamani, pia kuna wahalifu wanaojaribu kuiba thamani hiyo kwa faida yao binafsi.

Kuna njia mbili ambazo zina uwezekano mkubwa kutumiwa na wahalifu hawa kukudanganya:

- **Kukuuzia tokeni ya ulaghai**, ambayo inaweza kuonekana kama tokeni halali unayotaka kununua, lakini imetolewa na walaghai na haina thamani.
- **Kukuhadaa ili usaini miamala mibaya**, kwa kawaida kwa kukuelekeza kwenye kiolesura chao cha mtumiaji. Wanaweza kujaribu kukufanya utoe ruhusa kwa mikataba yao kutumia tokeni zako za ERC-20, jambo ambalo linaweza kufichua taarifa nyeti na kuwapa ufikiaji wa mali zako. Mara nyingi tovuti hizi hufanana kabisa na zile za halali, lakini zikiwa na ujanja uliojificha.

Ili kuonyesha tokeni za ulaghai ni nini, na jinsi ya kuzitambua, tutaangalia mfano mmoja: [`wARB`](https://eth.blockscout.com/token/0xB047c8032b99841713b8E3872F06cF32beb27b82). Tokeni hii inajaribu kufanana na tokeni halali ya [`ARB`](https://eth.blockscout.com/address/0xb50721bcf8d664c30412cfbc6cf7a15145234ad1).

<ExpandableCard
title="ARB ni nini?"
contentPreview=''>

Arbitrum ni shirika linalotengeneza na kusimamia [optimistic rollups](/developers/docs/scaling/optimistic-rollups/). Hapo awali, ilikuwa ni kampuni ya kibiashara yenye lengo la kupata faida, lakini baadae kuchukua hatua ya kugatua madaraka. Kama sehemu ya mchakato huo, walitoa [tokeni ya utawala](/dao/#token-based-membership) inayoweza kuuzwa.
</ExpandableCard>

<ExpandableCard
title="Mbona tokeni ya ulaghai inaitwa wARB?"
contentPreview=''>

Katika Ethereum, iwapo mali si ya kiwango cha ERC-20, huundwa toleo jipya ambalo limefungamana na kiwango hicho linaloanzia na herufi "w" kwenye jina lake. Kwa mfano, kuna wBTC kwaajili ya bitcoin na <a href="https://cointelegraph.com/news/what-is-wrapped-ethereum-weth-and-how-does-it-work">wETH kwaajili ya ether</a>.

Haileti maana kuwa na toleo la tokeni lililofungamana na kiwango cha ERC-20 kama tokeni tayari ni ya Ethereum, lakini matapeli hutegemea mwonekano wa uhalali badala ya ukweli wa msingi.
</ExpandableCard>

## Tokeni za udanganyifu hufanyaje kazi? {#how-do-scam-tokens-work}

Lengo kuu la Ethereum ni ugatuaji. Hii ina maana kwamba hakuna mamlaka ya kati inayoweza kukupokonya mali zako au kukuzuia kuunda mkataba wa kidijitali. Lakini pia ina maana kwamba matapeli wanaweza kuunda mikataba yoyote wanayotaka.

<ExpandableCard
title="Mikataba mahiri ni nini?"
contentPreview=''>

[Mikataba-erevu](/developers/docs/smart-contracts/) ni programu zinazoendeshwa juu ya blockchain ya Ethereum. Kila tokeni ya ERC-20, kwa mfano, huundwa kama mkataba wa kidigitali.
</ExpandableCard>

Hasa, Arbitrum ilipeleka mkataba unaotumia alama ya `ARB`. Lakini hilo halizuii watu wengine kuunda mikataba inayotumia alama hiyo hiyo au inayofanana. Yeyote anayeandika mkataba ndiye anayechagua mkataba huo ufanye nini.

## Kuonekana halali {#appearing-legitimate}

Kuna mbinu nyingi ambazo watengenezaji wa tokeni za udanganyifu hutumia ili kuonekana kama halali.

- **Jina na alama halali**. Kama tulivyosema awali, mikataba ya ERC-20 inaweza kutumia jina na alama sawa kabisa na mikataba mingine ya ERC-20. Hivyo basi, huwezi kutegemea majina au alama hizo kama kipimo cha usalama.

- **Wamiliki halali**. Mara nyingi, tokeni za ulaghai husambaza kiasi kikubwa cha tokeni kwa anuani ambazo zinatarajiwa kuwa wamiliki halali wa tokeni halisi.

Kwa mfano, hebu tuangalie `wARB` tena. [Takriban 16% ya tokeni](https://eth.blockscout.com/token/0xb047c8032b99841713b8e3872f06cf32beb27b82?tab=holders) zinashikiliwa na anwani ambayo lebo yake ya umma ni [Arbitrum Foundation: Deployer](https://eth.blockscout.com/address/0x1C8db745ABe3C8162119b9Ef2c13864Cd1FDD72F). Hii _sio_ anwani bandia, ni anwani halisi ambayo [ilipeleka mkataba halisi wa ARB kwenye Mtandao Mkuu wa Ethereum](https://eth.blockscout.com/tx/0x242b50ab4fe9896cb0439cfe6e2321d23feede7eeceb31aa2dbb46fc06ed2670).

Kwa sababu salio la ERC-20 la anuani fulani ni sehemu ya hifadhi ya mkataba wa ERC-20, mkataba unaweza kuamuliwa kuwa chochote msanidi anachotaka. Pia inawezekana mkataba kuzuia uhamishaji, hivyo watumiaji halali hawawezi kuondoa zile tokeni za udanganyifu.

- **Uhamishaji halali**. _Wamiliki halali hawangelipa kuhamisha tokeni ya ulaghai kwa wengine, kwa hivyo kama kuna hamisho, ni lazima iwe halali, sivyo?_ **Si kweli**. Matukio ya `Transfer` yanazalishwa na mkataba wa ERC-20. Tapeli anaweza kuandika mkataba kwa namna kwamba utazalisha vitendo hivyo kirahisi.

## Tovuti za ulaghai {#websites}

Matapeli wanaweza kutengeneza tovuti zinazoshawishi sana, mara nyengine hata nakala zinazofanana kabisa na tovuti za kweli na zenye muonekano sawa kabisa, lakini zote zikiwa ni njia za ujanja tu. Kwa mfano unaweza kuona kiungo cha nje kinachoonekana halali kabisa kumbe kinakupeleka kwenye tovuti ya kitapeli, au maelekezo yasiyo sahihi yanayokufanya utoe funguo zako au kutuma fedha kwenye anwani ya mshambuliaji.

Njia bora ya kujilinda na hili ni kukagua kwa makini URL ya tovuti unazotembelea, na kuhifadhi anuani za tovuti halisi kwenye vialamisho vyako. Ukifanya hivyo, utaweza kufikia tovuti halisi moja kwa moja kupitia vialamisho vyako bila kufanya makosa ya tahajia au kutegemea viungo vya nje.

## Unawezaje kujilinda? {#protect-yourself}

1. **Angalia anuani ya mkataba**. Tokeni halali zinatoka kwenye mashirika halali, na unaweza kuona anuani za mikataba kwenye tovuti rasmi ya shirika husika. Kwa mfano, [kwa `ARB` unaweza kuona anwani halali hapa](https://docs.arbitrum.foundation/deployment-addresses#token).

2. **Tokeni halisi zina ukwasi**. Chaguo jingine ni kuangalia ukubwa wa bwawa la ukwasi kwenye [Uniswap](https://uniswap.org/), mojawapo ya protokali za kawaida za kubadilisha tokeni. Itifaki hii inafanya kazi kwa kutumia mabwawa ya ukwasi, ambapo wawekezaji huweka tokeni zao wakitarajia kupata mapato kutokana na ada za biashara.

Tokeni za udanganyifu kwa kawaida huwa na mabwawa madogo sana ya ukwasi, au hayana kabisa, kwa sababu matapeli hawataki kuhatarisha mali halisi. Kwa mfano, bwawa la `ARB`/`ETH` la Uniswap lina takriban dola milioni moja ([angalia hapa kwa thamani ya sasa](https://app.uniswap.org/explore#/pools/0x755e5a186f0469583bd2e80d1216e02ab88ec6ca)) na kununua au kuuza kiasi kidogo hakutabadilisha bei:

![Kununua tokeni halali](./uniswap-real.png)

Lakini unapojaribu kununua tokeni ya ulaghai ya `wARB`, hata ununuzi mdogo ungebadilisha bei kwa zaidi ya 90%:

![Kununua tokeni ya ulaghai](./uniswap-scam.png)

Huu ni ushahidi mwingine unaoonyesha kuwa `wARB` kuna uwezekano si tokeni halali.

3. **Angalia kwenye Etherscan**. Tokeni nyingi za kitapeli tayari zimebainishwa na kuripotiwa na jamii. Tokeni kama hizi [zimetiwa alama katika Etherscan](https://info.etherscan.com/etherscan-token-reputation/). Ingawa Etherscan si chanzo rasmi cha ukweli (kwa sababu katika mitandao ambayo imegatuliwa hakuna chanzo kimoja cha ukweli), tokeni ambazo zimetambulika na Etherscan kama za kitapeli mara nyingi kweli huwa za kitapeli.

![Tokeni ya ulaghai katika Etherscan](./etherscan-scam.png)

## Hitimisho {#conclusion}

Almradi bado kuna thamani duniani, kutakuwepo na matapeli wanaotaka kuiba. Katika dunia ya kidijitali isiyo na udhibiti wa kati, hakuna wa kukulinda isipokuwa wewe mwenyewe. Ni matumaini yangu utayakumbuka mambo haya ili yakusaidie kutofautisha tokeni halali na za kitapeli:

- Tokeni za kitapeli huiga tokeni halali, zinaweza kutumia jina na alama sawa n.k.
- Tokeni za ulaghai _haziwezi_ kutumia anwani sawa ya mkataba.
- Chanzo bora cha anuani ya tokeni halali ni shirika linalomiliki tokeni hiyo.
- Ikishindikana, unaweza kutumia programu maarufu na za kuaminika kama vile [Uniswap](https://app.uniswap.org/#/swap) na [Blockscout](https://eth.blockscout.com/).
Original file line number Diff line number Diff line change
@@ -0,0 +1,75 @@
---
title: Jinsi ya Kubatilisha mkataba erevu usifikie fedha zako za kripto
description: Muongozo wa jinsi ya kuondoa mkataba mahiri unaofikiwa kidhalimu
lang: sw
---

# Jinsi ya Kubatilisha mkataba erevu usifikie fedha zako za kripto

Mwongozo huu utakufundisha jinsi ya kutazama orodha ya [smart contracts](/glossary/#smart-contract) zote ambazo umeziruhusu kufikia fedha zako na jinsi ya kuzighairi.

Wakati mwingine wasanidi programu wadanganyifu huweka milango ya siri kwenye mikataba mahiri ambayo inaruhusu kupata fedha za watumiaji wasiojua, ambao huingiliana na mkataba huo mahiri. Kinachotokea mara kwa mara ni kwamba mifumo kama hiyo humwomba mtumiaji ruhusa ya kutumia **idadi isiyo na kikomo ya tokeni** kwa jaribio la kuokoa kiasi kidogo cha [gesi](/glossary/#gas) siku zijazo, lakini hii huja na hatari iliyoongezeka.

Mara tu jukwaa linapokuwa na haki za ufikiaji zisizo na kikomo kwa tokeni kwenye [mkoba](/glossary/#wallet) yako, wanaweza kutumia tokeni hizo zote hata kama umetoa fedha zako kutoka kwenye jukwaa lao na kuzirudisha kwenye mkoba wako. Wafanya maovu bado wanaweza kufikia fedha zako na kuzitoa kuzipeleka hadi kwenye mikoba yao bila wewe kuwa na njia yoyote ya kuzirejesha.

Ulinzi pekee ni kujiepusha kutumia miradi mipya ambayo haijajaribiwa, idhinisha kile unachohitaji tu, au futa mara kwa mara ruhusa ulizozitoa awali. Sasa, jinsi gani unaweza fanya ivyo?

## Hatua 1: Tumia kifaa cha kubatilisha zana ya ufikiaji

Kuna tovuti kadhaa zinazokuwezesha kuona na kubatilisha mikataba mahiri iliyounganishwa na anwani yako. Tembelea tovuti na unganisha mkoba wako:

- [Etherscan](https://etherscan.io/tokenapprovalchecker) (Ethereum)
- [Blockscout](https://eth.blockscout.com/apps/revokescout) (Ethereum)
- [Revoke](https://revoke.cash/) (mitandao mingi)
- [Unrekt](https://app.unrekt.net/) (mitandao mingi)
- [EverRevoke](https://everrise.com/everrevoke/) (mitandao mingi)

## Hatua 2: Unganisha mkoba wako

Ukiwa tayari kwenye tovuti, bonyeza kwenye "Unganisha mkoba". Tovuti itakuletea wewe uunganishe mkoba wako.

Hakikisha kuwa unatumia mtandao mmoja kwenye mkoba wako na tovuti. Utaona tu mikataba mahiri inayohusiana na mtandao uliochagua. Kwa mfano, kama unaunganisha Ethereum Mainnet, utaona tu mikataba ya Ethereum, na sio mikataba kutoka kwenye minyororo mingine kama Polygon.

## Hatua 3: Chagua mkataba mahiri unaotaka kuubatilisha

Unatakiwa kuona mikataba yote ambayo imeruhusiwa kuunganishwa na tokeni zako na kiasi chake cha matumizi. Tafuta ule unaotaka kusitisha.

Kama hujui mkataba upi wa kuchagua, unaweza batilisha mikataba yote. Haitakuletea matatizo yoyote, lakini utahitaji kutoa ruhusa mpya tena wakati mwingine utakaposhirikiana na yoyote kati ya mikataba hii.

## Hatua 4: Batilisha ruhusa ya kuweza kufikia fedha zako

Mara tu unapobonyeza kubatilisha, unapaswa kuona pendekezo jipya la muamala kwenye mkoba wako. Hii ni ya kutarajiwa. Itabidi ulipe ada ili kufuta huko kufanikiwe. Kutegemea na mtandao, hii inaweza kuchukua kuanzia dakika moja hadi kadhaa ili kuchakatwa.

Tunakushauri uonyeshe upya chombo cha kubatilisha ruhusa baada ya dakika chache na kuunganisha tena mkoba wako ili kuangalia mara mbili kama mkataba uliotolewa umepotea kutoka kwenye orodha.

<mark>Tunapendekeza kamwe usiruhusu miradi ufikiaji usio na kikomo kwa tokeni zako na ughairi ruhusa zote za ufikiaji wa tokeni mara kwa mara. Kughairi ufikiaji wa tokeni kamwe hakupaswi kusababisha upotevu wa fedha, hasa ukitumia zana zilizoorodheshwa hapo juu.</mark>

<br />

<Alert variant="update">
<AlertEmoji text=":eyes:"/>
<AlertContent className="justify-between flex-row items-center">
<div>Unataka kujifunza zaidi?</div>
<ButtonLink href="/guides/">
Angalia miongozo yetu mingine
</ButtonLink>
</AlertContent>
</Alert>

## Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

### Je, kubatilisha ufikiaji wa tokeni pia kunakomesha kusindika, kuweka kwa pamoja kwenye bwawa, kukopesha n.k?

Hapana, haitaathiri mikakati yoyote ya [DeFi](/glossary/#defi) uliyonayo. Bado utabaki katika nafasi zako na kuendelea kupata zawadi n.k.

### Je, kukata muungano wa mkoba kutoka kwenye mradi ni sawa na kuondoa ruhusa ya kutumia pesa zangu?

Hapana, ukiondoa mkoba wako kwenye mradi, lakini tayari umetoa ruhusa ya kutumia tokeni, bado wanaweza kutumia tokeni hizo. Inakupasa kubatilisha ruhusa hiyo.

### Ruhusa ya mkataba itakwisha lini?

Hakuna tarehe ya mwisho wa matumizi kwenye ruhusa za mkataba. Kama utatoa ruhusa ya mkataba, zinaweza kutumika, hata miaka mingi baada ya kutolewa.

### Kwa nini miradi huweka ruhusa ya matumizi ya tokeni isiyo na kikomo?

Miradi mara nyingi hufanya hivi ili kupunguza idadi ya maombi yanayohitajika, ikimaanisha mtumiaji anapaswa kuidhinisha mara moja tu na kulipa ada ya muamala mara moja tu. Ingawa hii ni rahisi, inaweza kuwa hatari kwa watumiaji kuidhinisha bila uangalifu, hasa kwenye tovuti ambazo hazijathibitishwa na wakati au kukaguliwa. Baadhi ya mikoba hukuruhusu kuzuia mwenyewe kiasi cha tokeni zinazoidhinishwa ili kupunguza hatari yako. Wasiliana na mtoa huduma wa mkoba wako kwa maelezo zaidi.
70 changes: 70 additions & 0 deletions public/content/translations/sw/guides/how-to-swap-tokens/index.md
Original file line number Diff line number Diff line change
@@ -0,0 +1,70 @@
---
title: Jinsi ya kubadili tokeni
description: Muongozo wa jinsi ya kubadilisha tokeni kwenye Ethereum.
lang: sw
---

# Jinsi ya kubadili tokeni

Umechoshwa na kutafuta soko ambalo linaorodhesha tokeni zako zote uzipendazo? Unaweza kubadilishana tokeni nyingi kwa kutumia [masoko ya kubadilishana yasiyogatuliwa](/glossary/#dex).

Kubadilishana tokeni kunahusisha ubadilishanaji wa mali mbili tofauti zilizopo kwenye mtandao wa Ethereum, kwa mfano kubadilishana ETH kwa DAI (tokeni ya [ERC-20](/glossary/#erc-20)). Mchakato huu ni wa haraka na bei nafuu. Utahitaji kuwa na mkoba wa kripto kubadilisha tokeni.

**Vigezo vya Awali:**

- kuwa na [mkoba wa kripto](/glossary/#wallet); kama huna, unaweza kufuata mwongozo huu kuhusu [jinsi ya kufungua akaunti ya Ethereum](/guides/how-to-create-an-ethereum-account/)
- weka fedha kwenye mkoba wako

## 1. Unganisha mkoba wako kwenye soko la kubadilishana tokeni lililoondolewa mfumo wa kati (DEX) unalolipenda

Baadhi ya masoko maarufu ya kubadilishana ni:

- [Uniswap](https://app.uniswap.org/#/swap)
- [Sushiswap](https://www.sushi.com/swap)
- [1Inch](https://app.1inch.io/#/1/unified/swap/ETH/DAI)
- [Curve](https://www.curve.finance/dex/ethereum/swap/)

Inavutia? Jifunze zaidi kuhusu [fedha zilizogatuliwa (DeFi)](/defi/) ni nini na jinsi aina hizi mpya za masoko ya kubadilishana zinavyofanya kazi.

## 2. Chagua jozi ya tokeni unazotaka kubadilisha

Kwa mfano, ETH na DAI. Hakikisha una fedha kati ya mojawapo ya tokeni hizo mbili.
![Kiolesura cha kawaida cha kubadilishana](./swap1.png)

## 3. Ingiza kiasi cha tokeni unachotaka kubadilisha na bonyeza badilisha

Soko la kubadilishana litahesabu kiotomatiki idadi ya tokeni utakazopata.

![Kiolesura cha kawaida cha kubadilishana](./swap2.png)

## 4. Thibitisha muamala

Hakiki maelezo ya muamala. Kagua kiwango cha ubadilishaji na ada zingine zozote ili kuzuia mshangao mbaya.

![Kiolesura cha kawaida cha kukagua muamala](./swap3.png)

## 5. Subiri muamala uchakatwe

Unaweza kuona maendeleo ya muamala kwenye kipelelezi cha kiambajengo chochote. Mchakato huu hautakiwi kuchukua muda zaidi ya dakika 10.

Utapokea kiotomatiki tokeni ulizobadilisha kwenye mkoba wako mara tu muamala utakapochakatwa. <br />

<Alert variant="update">
<AlertEmoji text=":eyes:"/>
<AlertContent className="justify-between flex-row items-center">
<div>Unataka kujifunza zaidi?</div>
<ButtonLink href="/guides/">
Angalia miongozo yetu mingine
</ButtonLink>
</AlertContent>
</Alert>

## Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

### Je, ninaweza kubadilisha ETH kwa BTC kutoka kwenye mkoba wangu?

Hapana, unaweza tu kubadilisha tokeni ambazo ni za asili ya mtandao wa Ethereum, kama vile ETH, tokeni za ERC-20 au NFTs. Unaweza tu kubadilisha aina za Bitcoin zilizofungwa ambazo zinapatikana kwenye Ethereum.

### Slippage ni nini?

Ni tofauti kati ya kiwango chako cha ubadilishaji unachotarajia na kiwango halisi.
72 changes: 72 additions & 0 deletions public/content/translations/sw/guides/how-to-use-a-bridge/index.md
Original file line number Diff line number Diff line change
@@ -0,0 +1,72 @@
---
title: Jinsi ya kuvusha tokeni kwenda safu ya namba 2
description: Mwongozo unaoelezea jinsi ya kuhamisha ishara kutoka Ethereum hadi safu ya 2 kwa kutumia daraja.
lang: sw
---

# Jinsi ya kuvusha tokeni kwenda safu ya namba 2

Ikiwa kuna trafiki nyingi kwenye Ethereum, inaweza kuwa ghali. Suluhisho moja kwa hili ni kuunda "safu" mpya: yaani, mitandao tofauti ambayo inafanya kazi kwa njia zinazofanana na Ethereum yenyewe. Hizi zinazoitwa Tabaka 2 husaidia kupunguza msongamano na gharama kwa Ethereum kwa kuchakata miamala mingi zaidi kwa ada za chini, na kuhifadhi tu matokeo ya haya kwenye Ethereum kila baada ya muda fulani. Kwa hivyo, tabaka hizi za 2 hutuwezesha kufanya shughuli kwa kasi iliyoongezeka na gharama iliyopungua. Miradi mingi maarufu ya crypto inahamia safu ya 2 kwa sababu ya faida hizi. Njia rahisi zaidi ya kuhamisha tokeni kutoka Ethereum hadi safu ya 2 ni kutumia daraja.

**Vigezo vya Awali:**

- kuwa na mkoba wa crypto—kama huna, fuata mwongozo huu ili [kufungua akaunti ya Ethereum](/guides/how-to-create-an-ethereum-account/)
- weka fedha kwenye mkoba wako

## 1. Amua ni mtandao wa safu ya 2 ungependa kutumia

Unaweza kujifunza zaidi kuhusu miradi tofauti na viungo muhimu kwenye [ukurasa wetu wa safu ya 2](/layer-2/)

## 2. Nenda kwenye daraja liliyochaguliwa

Baadhi ya safu 2s maarufu ni:

- [daraja la Arbitrum](https://portal.arbitrum.io/bridge?l2ChainId=42161)
- [daraja la Optimism](https://app.optimism.io/bridge/deposit)
- [daraja la Boba Network](https://hub.boba.network/)

## 3. Unganisha kwenye daraja na mkoba wako

Hakikisha kuwa mkoba wako umeunganishwa kwenye mtandao wa Ethereum Mainnet. Ikiwa sivyo, tovuti itakuhimiza kiotomatiki kubadili mitandao.

![Kiolesura cha kawaida cha kuunganisha tokeni](./bridge1.png)

## 4. Taja kiasi na uhamishe fedha

Kagua kiasi ambacho utapata kwa kurudi kwenye mtandao wa safu ya 2 na ada ili kuepuka mshangao usio na furaha.

![Kiolesura cha kawaida cha kuunganisha tokeni](./bridge2.png)

## 5. Thibitisha muamala kwenye mkoba wako

Utalazimika kulipa ada (inayoitwa [gesi](/glossary/#gas)) katika mfumo wa ETH kwa ajili ya kuchakata muamala.

![Kiolesura cha kawaida cha kuunganisha tokeni](./bridge3.png)

## 6. Subiri pesa zako zihamishwe

Utaratibu huu haupaswi kuchukua zaidi ya dakika 10.

## 7. Ongeza mtandao wa safu ya 2 uliochaguliwa kwenye mkoba wako (hiari)

Unaweza kutumia [chainlist.org](http://chainlist.org) kupata maelezo ya RPC ya mtandao. Mara tu mtandao unapoongezwa na muamala kukamilika, unapaswa kuona tokeni kwenye mkoba wako. <br />

<Alert variant="update">
<AlertEmoji text=":eyes:"/>
<AlertContent className="justify-between flex-row items-center">
<div>Unataka kujifunza zaidi?</div>
<ButtonLink href="/guides/">
Angalia miongozo yetu mingine
</ButtonLink>
</AlertContent>
</Alert>

## Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

### “Itakuwaje kama nina fedha kwenye ubadilishaji?

“Huenda ukaweza kutoa fedha moja kwa moja kwenda kwenye baadhi ya safu 2s kutoka kwenye ubadilishaji.” Angalia sehemu ya "Hamia safu ya 2" ya [ukurasa wetu wa Safu ya 2](/layer-2/) kwa maelezo zaidi.

### “Je, naweza kurudi kwenye Ethereum mainnet baada ya kuhamisha tokeni zangu kwenda L2?”

“Ndiyo, unaweza kila wakati kuhamisha fedha zako kurudi kwenye mainnet ukitumia daraja lile lile.”
Loading